
WAKATI Rais Samia akiendelea kuhutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ghafla shangwe ziliibuka kutoka kona zote za ukumbi, baada ya kamera zilizomo ukumbini humo kumuonesha Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustine Mrema, ambaye ameambatana na mkewe Doreen.
Baada ya shangwe hizo, Rais Samia alionesha kushtuka kabla ya kubaini shangwe hizo zilisababishwa na muonekano wa Mrema na mkewa. Ndipo Rais akatamka “Bwana harusi hoyee” na kuitikiwa na ukumbi mzima oyeeee.“ Kisha Rais Samia akasema: Tuendelee.”
Mrema na mkewe waliofunga ndoa hivi karibuni katika Parokia ya Uwomboni, Jimbo Katoliki la Moshi, mkoani Kilimanjaro, waliibua shangwe hizo wakati wanaingia kwenye mkutano huo unaoendelea jijini Dodoma Ukumbi wa Mikutano wa CCM Jakaya Kikwete.