Mshindi wa Kwanza Kipindi cha Darasa Akabidhiwa Simu (Picha +Video)

MSHINDI wa Shindano la Jishindie Simu Janja (Smart Phone), Richard Boniphace, wa Tunduma Mbeya amepokelewa zawadi yake ya Simu janja aina ya Tecno Pop 2 Juni 22,2020 na Jimson Mwakalindile, kutoka kwa walimu wanaoendesha kipindi hicho cha Darasa, Eric Shigongo na Rodric Nabe katika ofisi za Grobal Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Huyu anakuwa mshindi wa kwanza kupewa zawadi ya simu baada ya droo ya kwanza kuchezwa Juni 16, 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group Eric Shigongo na mwalimu wa kipindi hicho baada ya kukabidhi zawadi kwa mshindi huyo, amewahimiza Watanzania kuendelea kufuatilia kipindi hicho cha Darasa kinachorushwa na Global Radio na Global TV Online, kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia Saa 10:00 hadi saa 11:00 jioni.

Naye mwalimu Nabe, amewapongeza washiriki wote wanaoendelea kushiriki shindano hilo na kuwataka waendelee kufuatilia kipindi hicho bila kusahau ku-comment, ku-subscribe na kuacha namba zao za simu wakati kipindi cha Darasa kikiendelea Global TV Online.

Baada ya kupokea zawadi hiyo kwa niaba ya Boniphace, Mkwakalindile alisema kuwa ni jambo jema kuendesha kipindi hicho cha Darasa ambacho kimekuwa kikiwabadilisha mitazamo watu wengi wanaofuatilia kipindi.
Shindano bado linaendelea kwa ambao wanahitaji kushiriki na ili kujishindia zawadi mbalimbali wasisahau kutazama kipindi hicho kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa, KUANZIA SAA 10:00 MPAKA SAA 11:00 JIONI.

Ili kwenda sambamba na shindano hili, fanya hivi; Ingia YouTube Channel ya Global TV kisha, Subscribe na Bonyeza alama ya kengele 🔔 (Notification bell). Kipindi kinapokuwa hewani, ingia kwenye LIVE CHART kisha comment na uandike namba yako ya simu.
Watu 100 wa kwanza wataingia kwenye droo ya kujishindia zawadi mbalimbali kila wiki.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

