Mti wa Ajabu kwa ‘Babu Tale’, Unakusanya Kijiji Kizima – Video

MATULI ni kijiji kilichopo Ngerengere mkoani Morogoro, Jimbo la Morogoro Kusini-Mashariki chini ya Mbunge wake, Hamis Taletale (Babu Tale).
Kijiji hiki kina wakazi takribani 5,000 na miongoni mwa changamoto kubwa zinazokikabili ni miundombinu ya wawasiliano
Kijiji hiki kimegundulika mti mmoja ambapo simu zote zinapatikana hapo, hali iliyofanya wanakijiji hao kuupenda ili kufanya mawasiliano ya simu na jamaa zao walio nje ya kijiji hicho.
Ili mtandao ukamate, wanakijiji wanasema mtu anahitajika kuweka simu yake kwenye moja ya makopo yaliyotundikwa hapo ili kupata mawimbi ya mitandao.

