The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mtoto Auawa Katika Jaribio la Kuzuia Risasi kwa Kutumia Hirizi

0
Kijana ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akijaribu kuizuia kwa njia ya hirizi

Mtoto mwenye umri wa miaka 12, anayefahamika kwa jina la Yusuph Abubakari ameuawa baada ya kaka yake, Abubakari Abubakari kujaribu kumpiga risasi huku akidhani kuwa hirizi mpya aliyoivaa itamlinda.

 

Polisi wa Nigeria wametoa taarifa hiyo na kueleza kuwa mtuhumiwa tukio hilo alimpiga risasi mdogo wake kwa kutumia bunduki ya baba yake.

 

Aidha, Polisi wamesema kuwa Yusuf Abubakar alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa risasi huku kaka yake, Abubakari Abubakari akitorokea msituni na haijabainika kwa nini ndugu hao wawili walienda kupata ulinzi kwa kutumia hirizi.

Askari Polisi wanamsaka mtuhumiwa wa mauaji

Polisi kwa sasa wanamtafuta mtuhumiwa wa mauaji na kueleza kuwa bunduki iliyotumika katika kutekeleza mauaji hayo ni ya kizamani inayojulikana kwa jina la dane gun.

Kijana ameuawa na risasi kwa kutegemea nguvu ya hirizi

Pia, Polisi wameeleza kuwa baba wa watoto hao anafanya shughuli za uwindaji na kuwataka wazazi kufuatilia shughuli za watoto wao na kuepuka kufanya shughuli zisizofaa.

 

Taarifa zinadai kuwa katika Nchi ya Nigeria hirizi hutumiwa na baadhi ya watu ambao wanataka ulinzi dhidi ya matukio mabaya na kwamba kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kuuawa baada ya kupima hirizi na dawa za kishirikina za kuzuia risasi.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply