The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mwanamke Aliyedhaniwa Amefariki Azinduka Ndani ya Jeneza Thailand

0

Mwanamke mmoja nchini Thailand aliwashangaza na kuwaogopesha wafanyakazi wa hekalu baada ya kuanza kusogea akiwa ndani ya jeneza lake akiwa tayari amefikishwa kwa ajili ya kuchomwa moto.

Tukio hilo limetokea katika Hekalu la Wat Rat Prakhong Tham, lililopo jimbo la Nonthaburi, nje kidogo ya Bangkok. Video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa hekalu hilo inaonyesha mwanamke huyo akiwa amelala kwenye jeneza jeupe nyuma ya lori, akionyesha kusogeza mikono na kichwa, hali iliyowaacha watumishi wa hekalu wakiwa katika zo kubwa na mshangao.

Pairat Soodthoop, meneja mkuu wa masuala ya fedha wa hekalu hilo, ameiambia shirika la habari la Associated Press kuwa kaka wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 65 alimleta kutoka Mkoa wa Phitsanulok akiamini kuwa alikuwa tayari amefariki dunia.

Pairat alisema walianza kusikia mlio ukitoka kwenye jeneza.

“Nilishangaa, nikawaomba wafungue jeneza. Kila mtu alishtuka. Tulimwona akifungua macho yake kidogo na kugonga upande wa jeneza. Inaonekana alikuwa akigonga kwa muda,” alisema.

Kwa mujibu wa Pairat, kaka wa mwanamke huyo aliwaeleza kuwa dada yake alikuwa amelazwa kitandani kwa takriban miaka miwili, na hali yake ya afya ilizorota kiasi kwamba siku mbili zilizopita aliacha kupumua kabisa, hivyo familia ikaamini amefariki.

Baada ya kudhani kuwa amekata roho, kaka huyo alimuweka kwenye jeneza na kuanza safari ya zaidi ya kilomita 500 hadi Bangkok, ambako mwanamke huyo alikuwa amewahi kueleza kuwa angependa kutoa viungo vyake kusaidia wengine.

Leave A Reply