The House of Favourite Newspapers
gunners X

Video: Mwenyekiti wa Mtaa wa Oysterbay Aeleza Mtego Uliowanasa Wachina

0

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Mololo Mwaisumo, ameuelezea umma namna walivyofanikiwa kuwaweka mtegoni na kuwanasa raia wawili wa China waliokuwa wakihifadhi maburungutu ya fedha ndani ya chumba wanachoishi.

Akizungumza na Global TV, Mwaisumo amesema tukio hilo lilitokana na ufuatiliaji wa kina uliofanywa kwa ushirikiano wa viongozi wa mtaa na vyombo vya usalama, baada ya kupata taarifa za kiashiria cha uwepo wa shughuli zisizo za kawaida katika eneo hilo.

Ameeleza kuwa viongozi wa mtaa walianza kuwafuatilia watu hao kwa muda, huku wakikusanya taarifa muhimu hadi pale mtego ulipowekwa na kufanikiwa kuwanasa wakiwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichohifadhiwa katika chumba walichokuwa wakiishi.

Mwaisumo ameongeza kuwa baada ya kukamatwa, raia hao wa China walikabidhiwa kwa vyombo vya dola na tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ambako wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi.

Leave A Reply