The House of Favourite Newspapers
gunners X

Nabii Aliyetabiri Ajali ya Ndege Bukoba Wiki Mbili Kabla ya Kutokea – Video

0

Taifa la Tanzania linaomboleza vifo vya watu 19 huku wengine 24 wakiokolewa hai kufuatia ajali mbaya ya ndege ya Shirika la Precision Air iliyotokea juzi Jumapili, Novemba 6, 2022 katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba kutokana na hali ya hewa.
Mtumishi wa Mungu, Pastor Malachi amewashangaza wengi baada ya video yake kusambaa ikimwonyesha akitoa unabii juu ya ajali hiyo ya ndege takribani wiki zilizopita kabla ya ajali kutokea.

Mchungaji huyo wa Kanisa la Christ Mandate alitoa unabii huo kwenye ibaada maalum na maombi Oktoba 20, 2022, katika Kanisa hilo lililopo Kigogo, jijini Dar es Salaam mkabala na Kituo cha Polisi Kigogo na kusema;

“Ilikuwa Oktoba 20, nilitoa unabii kuhusu janga la ndege ama ajali ya ndege, Idara ya Matangazo onyesheni kilichotokea leo Ziwa Victoria… kama si maombi yetu siku ile, ndiyo maana unahitaji kuwa na nabii,” alisema Pastor Malachi.

Siku ya unabii (Oktoba 20, 2022) ilivyokuwa;

“Inua mkono wako juu, nilikuwa nataka kushusha hii maiki (kipaza sauti) lakini Bwana akasema futa mauti. Sema kama nimewekewa alama ya umauti kwenye familia yangu, kupitia ajali… pia ninaona ndege ikianguka, tunaenda kufuta. Sema Eee Bwana, tunaporomosha mimba ovu, za vifo vya ghafla kwenye familia zetu,” Pastoer Malachi alitoa unabii na kukemea.

Baada ya kutoa nabii hiyo, Pastor Malachi ambaye amekuwa maarufu kwa kutoa mapepo, kuharibu nguvu za giza zilizokufunga, magonjwa sugu kama kisukari na presha, aliwaongoza waumini wote katika kuliombea tifa na kulikabidhi mikononi mwa Mungu ili kuepukana na mauti ambayo yangesababishwa na ajali hiyo.

Leave A Reply