The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ndege ya Kijeshi ya Marekani, Osprey Yaanguka Baharini, Yaua Mtu mmoja

0

Mtu mmoja amefariki dunia huku wengine wakiwa hawajulikani walipo baada ya ndege ya kijeshi ya Marekani, Osprey kuanguka baharini Kusini mwa Japan, tukio lililotokea asubuhi ya Jumatano, Novemba 29, 2023.

Mamlaka zimeeleza kuwa ajali hiyo imetokea jirani na Kisiwa cha Yakushima imeelezwa kuwa taarifa za awali kutoka Kitengo cha Air Force Special Operations Command zikieleza kuwa ndege hiyo ilikuwa na watu nane wakati ikipata ajali.

Vikosi vya uokoaji vimeeleza kuwa mwanaume mmoja alipatikana baharini akiwa hajitambui, karibu na eneo la ajali upande wa Mashariki mwa Yakushima ambapo alisafirishwa mpaka katika Bandari ya Anbo ambapo baadaye ilibainika kwamba amefariki dunia huku kukiwa hakuna maelezo ya haraka juu ya hali ya ndege au wengine waliokuwemo.

CCM KWAFUKUTA /CHONGOLO AKUBALIWA KUJIUZULU /KIGOGO ATOA PESA KUPATA UBUNGE /POLISI MBARONI

Leave A Reply