The House of Favourite Newspapers

Neymar Afunguka Sababu ya Kulia

0

STAA wa Brazil, Neymar amesema kuwa alimwaga machozi baada ya mchezo wa Copa Amerika kwa kuwa Wabrazili wote walikuwa nyuma yao.

 

Wikiendi iliyopita Brazil na Argentina walivaana kwenye fainali ya Copa Amerika, ambayo ilipigwa kwenye Dimba la Maracana na kushuhudia Argentina wakipata ushindi wa bao 1-0.

 

Bao pekee la Argentina lilifungwa na kiungo wa PSG, Angel di Maria kipindi cha kwanza na kupoteza kabisa nguvu ya Brazil ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huu.

 

Neymar baada ya mchezo kumalizika alijikuta akitokwa na machozi baada ya kushuhudia Argentina chini ya staa wao Lionel Messi wakishangilia kutwaa ubingwa huo muhimu kwao.

 

“Sikulia kwa ajili yangu nilikuwa nawatazama mashabiki, machozi yananitoka, kila mmoja alionyesha kuwa anaitakia mema timu hii, hiki ndiyo kiliniliza” alisema Neymar juziHuu umekuwa ubingwa wa kwanza mkubwa kwa Messi akiwa na timu hiyo ya Taifa, baada ya kuwa ameshatwaa makombe yote makubwa ya ngazi ya klabu .

Leave A Reply