Neymar Jr Hatihati Kuikosa Fainali UEFA
STAA wa Paris Saint Germain, Neymar Jr huenda akakumbana na adhabu kutoka UEFA baada ya kubadilishana jezi na mchezaji wa RB Leipzig ikiwa amevunja sheria za kujikinga na Virusi vya Corona.Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kati ya PSG na RB Leipzig.
Katika mchezo huo Neymar alibadilisha jezi na Marcel Halstenberg.Imeelezwa kuwa Neymar yupo hatarini kuambulia adhabu ya kufungiwa kwa sasa amevunja sheria za jinsi ya kujizuia na Virusi vya Corona.
UEFA ilitoa maelekezo katika michuano hiyo wachezaji hawataruhusiwa kubadilishana jezi baada ya mechi na ambaye atafanya hivyo basi atakosa mechi moja na atajitenga kwa siku 12.
Hivyo, kuna uwezekano mkubwa PSG ikamkosa staa wake huyo kwenye fainali ambayo watacheza na Bayern Munich au Lyon siku ya Jumapili.
PSG, juzi ilitinga fainali mbele ya RB Leipzig baada ya kushinda kwa mabao 3-0. Mabao kwenye mchezo huo yalifungwa na Marquinhos, Angel Di Maria na Juan Bernat.Neymar hakufunga bao lolote, lakini alifanya kazi kubwa akiwa kwenye kiwango cha juu na kuisaidia timu hiyo



