
Katika mazingira ya uchumi wa Tanzania, kumiliki gari ni jambo linaloonekana kuwa la kifahari, lakini ukweli ni kwamba hata mtu wa kipato cha chini anaweza kumiliki gari endapo atachagua kwa umakini aina ya gari, gharama za matumizi, na mpango sahihi wa kifedha.
Gharama kuu zinazofanya gari liwe gumu kumiliki ni:
Gharama kuu zinazofanya gari liwe gumu kumiliki ni:
-
Bei ya ununuzi
-
Matumizi ya mafuta
-
Upatikanaji wa spea
-
Gharama ya matengenezo
-
Bima, service na leseni
Kwa kuzingatia mambo hayo, hizi ndizo aina 10 za magari rafiki kwa mtu wa kipato cha chini.
1. Toyota Vitz (1.0 – 1.3 CC)
Kwa nini inafaa?
-
Matumizi madogo sana ya mafuta
-
Spea zinapatikana kila kona
-
Bei ya kununua si kubwa (kuanzia TSh 8m – 14m)
-
Matengenezo yake ni nafuu
Bora kwa:
Wafanyakazi wapatao mshahara mdogo, wanafunzi, na watu wanaohitaji usafiri wa kila siku mjini.
2. Toyota IST
Kwa nini inafaa?
-
Inatumia mafuta kidogo
-
Imara kuliko Vitz
-
Spea nyingi na rahisi
-
Bei: TSh 12m – 20m
Bora kwa:
Mtu wa kipato cha chini anayetaka gari dogo lakini imara.
3. Toyota Passo
Faida zake:
-
Bei rafiki (8m – 12m)
-
Matumizi ya mafuta chini
-
Spare parts nyingi kwenye soko
4. Suzuki Alto / Spacia / Wagon R
Kwa nini hizi gari ni bora?
-
Kei car — zinatumia mafuta kidogo zaidi kuliko nyingi
-
Bei zake ziko chini (7m – 12m)
-
Matengenezo ya bei nafuu
5. Toyota Probox / Succeed
Faida:
-
Ina nguvu zaidi
-
Ina beba mizigo
-
Matumizi ya mafuta ni ya wastani
-
Bei: 13m – 20m
6. Toyota Corolla (Old models: 110/120)
Kwa nini ni chaguo zuri?
-
Gari imara sana
-
Spea zinapatikana kwa bei ndogo
-
Mafuta si mengi (1.5 – 1.8cc)
-
Bei: 6m – 12m
7. Nissan March
Faida:
-
Inatumia mafuta kidogo
-
Bei ya ununuzi ni nafuu (6m – 10m)
8. Honda Fit
Faida:
-
Ina nafasi kubwa kuliko magari madogo
-
Inatumia mafuta kidogo
-
Bei: 9m – 15m
9. Toyota Raum
Kwa nini inafaa?
-
Ni spacious, ina nafasi kubwa
-
Matumizi mazuri ya mafuta
-
Bei: 10m – 15m
10. Toyota Noah (Old Models)
Faida:
-
Ina beba familia nzima
-
Matengenezo yake ya zamani si makubwa
Bei:
Kuanzia 9m – 15m (kutegemea model)
Bora kwa:
Familia kubwa au matumizi ya biashara (ushauri: mtumiaji awe tayari na bajeti ya mafuta kidogo juu).

