
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimetangaza nafasi mbalimbali za ajira kwa kada ya Tutorial Assistant katika fani tofauti, kwa lengo la kuimarisha rasilimali watu na kutekeleza dhamira ya kutoa elimu bora, rahisi na inayopatikana kwa wote.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa Desemba 10, 2025, OUT inahitaji wataalamu wenye sifa stahiki kwa vituo vyake vya kikanda na makao makuu yaliyopo Dar es Salaam, pamoja na vituo vya Arusha, Mtwara, Handeni, Kahama, Kigoma, Mbeya na Rukwa.
Soma zaidi hapa >>>TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
Nafasi Zilizotangazwa
Nafasi za Tutorial Assistant zimetangazwa katika fani zifuatazo:
-
Social Work
-
Psychology
-
History
-
Human Resource Management
-
Economics and Statistics
-
Finance and Accounts
-
Cybersecurity
-
Textile Design and Technology
-
Physics
-
Educational Management
-
Early Childhood Education
-
Curriculum and Instruction
-
Jurisprudence
-
Tax Law
-
International Law
Kila nafasi ni post 1, na waombaji watakaofanikiwa watahitajika kuendelea na masomo ya Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) kama sehemu ya mafunzo ya kazi.
Sifa Kuu za Waombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa:
-
Raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45
-
Mhitimu wa Shahada ya Kwanza husika kutoka chuo kinachotambuliwa
-
Awe na GPA isiyopungua 3.8 kati ya 5
-
Awe tayari kushiriki katika ufundishaji, tafiti na shughuli za kitaaluma
Mshahara
Mishahara italipwa kwa mujibu wa PUTS 1.1.

Soma zaidi hapa >>>