The House of Favourite Newspapers
gunners X

Pigabet Yawatangaza Washindi wa Promosheni za Shinda Ndinga na Jismatishe

0

Kampuni ya michezo ya kubashiri PigaBet leo imetangaza kwa shangwe majina ya washindi wa promosheni zake kubwa mbili – SHINDA NDINGA na JISMATISHE, katika droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa promosheni ya SHINDA NDINGA ni Musa Nicodemus kutoka mkoa wa Mwanza, ambaye ameibuka na zawadi ya smartphone ya kisasa kupitia kampeni hiyo ya kipekee.

Washindi wa JISMATISHE

Hamis Kassim kutoka Tegeta, Dar es Salaam – amejinyakulia Smart TV aina ya Hisense yenye ukubwa wa inch 55.

Innocent Sanga kutoka Arusha – ameibuka mshindi wa smartphone ya kisasa aina ya Samsung.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa washindi, Meneja Mawasiliano wa PigaBet, Hemed Jaafary Msonge, alisema:

“Tunafurahi kuona wateja wetu wakiendelea kufurahia promosheni zetu na kushinda zawadi kubwa. Hii ni njia yetu ya kurudisha shukrani kwa wachezaji wote wanaotuamini kila siku.”

Leave A Reply