Polisi Manyara: Mchungaji Mtaita hakutekwa tunamshikilia kwa Uchochezi – Video

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linamshikilia Mchungaji Eleth Mtaita wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boay, Wilaya ya Babati, kwa tuhuma za kuwahamasisha waumini kutoshiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani, amethibitisha kukamatwa kwa mchungaji Mtaita siku ya Ijumaa, Oktoba 24, 2025, na kueleza kuwa anahojiwa kuhusu madai hayo.
Aidha, Polisi wanamsaka Sheikh Juma Silima kutoka msikiti wa eneo hilo, ambaye naye anatuhumiwa kuhamasisha wananchi kutoshiriki kupiga kura.
Kamanda Makarani pia amewatahadharisha viongozi wa dini kutojihusisha na masuala ya kisiasa, akisisitiza kuwa nyumba za ibada zinapaswa kubaki kuwa maeneo ya kuabudu na si majukwaa ya harakati za kisiasa.


