Polisi Morogoro Wafuatilia Kutoweka kwa Mtawa Silianus Korongo – Video

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linafuatilia taarifa za kutoweka kwa Mtawa aliyetambulika kwa jina la Silianus Korongo (49) Mkazi wa Mtaa na Kata ya Tungi, Manispaa ya Morogoro, ambaye ametoweka katika nyumba ya malezi ya Watawa wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Franciscan (ORDER OF FRIARS MINOR -OFM ) tangu Disemba 1, 2025.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, aliyoitoa Disemba 3, 2025 imeeleza kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa za kutoweka kwa Mtawa huyo, ikieleza kwamba mara ya mwisho alitoka kwa ajili ya kwenda kununua Vifaa vya Ujenzi na hakurejea
Kamanda Mkama amesema uchunguzi na ufuatiliaji unaendelea, huku Jeshi hilo likitoa wito kwa Mwananchi yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kuhusu kutoweka kwa Mtawa huyo kuwasilisha taarifa hizo katika kituo chochote cha Polisi.


