Polisi Tarime Rorya Wakanusha Taarifa za Kutekwa kwa Mkazi wa Gwitiryo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya limekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kutekwa kwa Fredrick Mang’era Kemange maarufu British, mkazi wa Kijiji cha Gwitiryo Sirari likieleza kuwa linamshikilia kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uchochezi na kuhamasisha vurugu Desemba 09, 2025.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema British amekamatwa Desemba 03, 2025 majira ya saa saba mchana akiwa hotelini na kufikishwa kituo cha polisi Sirari kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha, Jeshi la Polisi limesema litaendelea kuwasaka na kuwakamata wale wanaoendesha makundi mbalimbali, kuchapisha na kusambaza taarifa zenye maudhui ya kuhamasisha uhalifu katika mitandao ya kijamii.




