The House of Favourite Newspapers

Polisi Waanza Uchunguzi wa Video ya Askari Kulala Chini – Video

0

Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi mara moja juu ya video iliyoenea mitandaoni ikimuonyesha askari mmoja amelala chini.

Taarifa iliyotolewa Septemba 24, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, imesema kuwa polisi wanatafuta mtu aliyerekodi video hiyo pamoja na aliyeandaa maneno yaliyoambatana nayo.

Video hiyo iliibuka kwenye mtandao wa Instagram, ikiwa imeshirikishwa na Mwanaharakati Mange Kimambi, ambapo ilichanganywa na maelezo yanayodai kuwa askari wananyanyaswa na OCS wa Kituo cha Polisi cha Bandari.

Hata hivyo, polisi wamesisitiza kuwa askari anayeonekana kwenye video yuko chumba cha mahabusu bila kosa lolote, na kuwekwa humo kutokana na kukataa kutoa rushwa.

DCP Misime ameongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini ukweli wa video hiyo na masharti yote yanayohusiana nayo.

Leave A Reply