The House of Favourite Newspapers

Video: Polisi Wafunguka Tukio la Kutoweka kwa Padri wa Jimbo Kuu la Songea

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linaendelea na uchunguzi wa tukio la kupotea kwa Padre Camillus Nikata, wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, amesema kuwa Padre Nikata alifika Songea tarehe 03 Oktoba 2025, akitokea Dodoma, akiwa na mhadhiri mwenzake ambaye pia ni Padre wa Jimbo la Songea, na walipofika walikaa katika Nyumba ya Mapadre ya St. Shanney.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mnamo tarehe 07 Oktoba 2025 majira ya jioni, Padre Nikata alionekana kwa mara ya mwisho na Padre mwenzake katika Mtaa wa Kanisani, akiwa na kibegi kidogo mkononi, akielekea Stendi ya Zamani ya Mabasi Mfaranyaki. Tangu siku hiyo, hajarejea alipokuwa amefikia.

Baada ya jitihada za awali za kumtafuta katika maeneo mbalimbali kutofanikiwa, tarehe 09 Oktoba 2025, Kanisa na Mapadre wenzake walitoa taarifa rasmi kwa Polisi kuhusu kutoweka kwake.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini alipo Padre Camillus Nikata pamoja na mazingira halisi ya kutoweka kwake.

Leave A Reply