PSSSF Kuimarisha Uhusiano na Global Group, Yaadhimia Kutoa Elimu ya Mfuko

MENEJA Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Ndugu James Mloe, ametembelea Ofisi za Global Group jijini Dar es salaam kwa lengo la kudumisha ushirikiano na vyombo vya habari katika kutoa elimu na taarifa mbalimbali za mfuko.

Katika ziara hiyo fupi, ndugu Mloe, ambaye aliongozana na Ofisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo, Ndugu Abdul Njaidi, alikutana na kufanya mazungumzo mafupi na Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho, Alhamisi Okt 7, 2022.