The House of Favourite Newspapers
gunners X

Rais Samia Afungua Kituo Cha Biashara Na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 1, 2025, amefungua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (East African Commercial and Logistics Centre – EACLC) kilichopo eneo la Ubungo, Dar es Salaam.

Kituo hicho kimelenga kuwa kiungo muhimu cha kuimarisha biashara, usafirishaji na usambazaji wa bidhaa ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, sambamba na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha kimkakati cha biashara katika kanda.

EACLC kinatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji, ajira, na uwekezaji, huku kikitoa huduma za kisasa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Rais Dkt. Samia akiwa na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC).
Rais Samia akiwa kwenye ufunguzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC).

Rais  Samia akitembelea maduka yaliyopo katika Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2025.

 

Comments are closed.