
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo kufutia kifo cha Waziri wa Ulinzi, Elias Kwandikwa, aliyefariki dunia jana Jumatatu, jijini Dar es Salaam. Pichani ni Rais Mwinyi na Kwandikwa, wakiwa Ikulu ya Zanzibar.


