The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Asema Mkoa wa Tabora Utakuwa Kitovu cha Biashara, Asifia Miundombinu Yake

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Mkoa wa Tabora unatarajiwa kuwa kitovu cha biashara kutokana na kuunganishwa na miundombinu mizuri inayoufanya mkoa huo kuwa na urahisi wa mawasiliano kwa mikoa mingine inayoizunguka.

 

Rais Samia ameyasema hayo wakati wa kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa reli ya SGR ambao mkoa wa Tabora nao ni miongoni mwa Mikoa inayotarajiwa kunufaika na mradi huo.

 

Rais Samia amesema Mkoa wa Tabora unatarajiwa kuwa kitovu cha biashara nchini

 

Aidha Rais Samia ametoa rai kwa mamlaka husika kutowazungusha wawekezaji hasa pale wanapokuja kuwekeza nchini na kushauri mamlaka hizo kufanya kazi na kuwajibika kwa haraka ili kutowakatisha tamaa wawekezaji kwani kwa sasa dunia ina ushindani mkubwa wa kibiashara hivyo wawekezaji wakizungushwa huamua kuondoka na kwenda sehemu nyingine.

 

Rais Samia ametoa rai kwa Watanzania kutunza miundombinu ambayo serikali inagharamia kwa pesa nyingi.

 

Kwa upande mwingine, Rais Samia amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia upya sheria za PPP na sheria za manunuzi kuona namna ambavyo zinaweza kufanyiwa marekebisho hasa pale linapotokea suala la kutoa zabuni au kusaini mikataba kwa wawekezaji ambao wanaonekana wana tija kuliko kusubiri mlolongo mrefu ambao mwisho wa siku huwakatisha tamaa wawekezaji na kutengeneza mianya ya rushwa.

 

Leave A Reply