The House of Favourite Newspapers

Afande Sele: Ni Laana Kumdharau Mama Aliyekuzaa kwa Upasuaji

0
Afande Sele Rapa Mkongwe nchini Tanzania

AFANDE SELE; ni rapa mkongwe wa kutema mistari ya muziki kutoka nchini Tanzania ambaye hatimaye amezungumzia tatizo la kiafya ambalo limekuwa likimtatiza kwa muda mrefu na pia kuwatetea kina mama wanaojifungua kwa njia ya upasuaji.

 

Afande Sele ameachia ujumbe mrefu ambapo amezungumza kwa kina jinsi amekuwa akitaabika kupata matibabu baada ya upasuaji ambapo amewasifia kina mama wanaozaa kupitia njia ya upasuaji na kufutilia mbali dhana inayoenezwa kwamba wao hawajifungui kwa uchungu.

 

Mfalme huyo wa mistari anasema; “Hujafa hujaumbika na afichae maradhi mauti humuumbua lakini cha mno zaidi husema kuugua ni moja ya ibada kwenye ramani ya maisha yetu wanaadamu chini ya jua.

 

“Majuzi wakati nikiwa ndani ya chumba cha upasuaji tatizo langu la hernia ambalo mara nyingi hutusumbua kuliko wavulana nilijifunza jambo kubwa kiasi cha kuona ni muhimu niwajuze akina ndugu hasa wa kizazi wasiendelee kuamini kile wanachoaminishana siku hizi mitaani hadi kuwafanya baadhi yao kuanza kuwachukulia poa mama zao waliowazaa…”

 

Rapa huyo analizamia ndani zaidi suala linalotembezwa mitaani kwamba wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji hawapitii uchungu halisi wa kujifungua kisa wanachomwa sindano ya ganzi na huwa hawahisi.

 

Anasema kwamba baada ya kupitia upasuaji wa kutibu ugonjwa wake wa hernia, njia hiyo ya upasuaji pia ni uchungu hata kuzidi kule kuzaa kwa kawaida na kuwataka watu kutowachukulia kina mama poa na kuwapa heshima yao.

Afande Sele ametoa pongezi kwa Wanawake wanaojifungua kwa upasuaji

“Inaeleweka wazi kuwa mabadiliko ya mazingira ya dunia ya leo katika mambo mengi yanachangia wakina mama wengi kujifungua watoto wao Kwa njia ya upasuaji badala ya ile njia ya asili kama viumbe wengine…Hali hiyo imepelekea huku kitaani kuzuka uzushi kuwa wamama wa leo hawazai kwa uchungu kwani kupitia njia ya upasuaji eti wanachomwa sindano ya ganzi hivyo hawaskii uchungu wowote mtoto anapotolewa tumboni na madaktari kama inavyokua kwenye kuzaa kwa njia ya kawaida au ya asili.

 

“Mimi binafsi na wanaume wenzangu ambao tumewahi kupitia mapito haya ya kufanyiwa upasuaji tunayo nafasi kubwa ya kuwaelimisha wavulana wetu wengi wanaozidi kuambukizana imani hiyo ya uongo ili kuepusha laana za wazazi kwa watoto wao wenye imani hiyo inayowasababisha kuanza kuwadharau mama zao kwenye safari ya maisha…Ukweli ni kwamba kupitia upasuaji wanachomwa ganzi lkn ganzi siyo jambo la kudumu kwani huisha na baada ya hapo wao hubaki na kidonda ambacho huendelea kuwapa maumivu na kujiuguza kwa muda mrefu pengine kuzidi wale wanaotumia njia ya kawaida,” anamalizia Afande Sele.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply