Rais Samia Afanya uteuzi na kumpangia balozi kituo cha kazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Majaba Shabani Magana kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) akichukua nafasi ya Bi. Fatma Ayoub Mwinyimvua Simba. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Magana alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa, Benki ya Azania; na
Vilevile kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amempangia Balozi Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria. Balozi Kakele anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Benson Alfred Bana ambaye amestaafu.