The House of Favourite Newspapers
gunners X

Rais Samia Aizawadia Taifa Stars Milioni 500 Baada ya Kufuzu 16 Bora AFCON

0

Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeizawadia timu ya Taifa (Taifa Stars) kiasi cha shilingi milioni 500 kama pongezi kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taarifa hiyo imetolewa leo, Januari 3, 2026, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza kwa njia ya simu na wachezaji pamoja na benchi la ufundi, baada ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Dkt. Nchemba amesema Mheshimiwa Rais amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria, huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuiunga mkono timu hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia ameahidi kutoa zawadi nyingine nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco.

Leave A Reply