Rais Samia Amrejesha Nyumbani Balozi Nchimbi, Ahamisha Vituo Vya Kazi Mabalozi 4

Balozi Emmanuel J. Nchimbi amerejeshwa nyumbani kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini Misri na nafasi yake inachukuliwa na Balozi Meja Jenerali Richard M. Makanzo
Ali J. Mwadini anakuwa Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa akichukua nafasi ya Balozi Dkt. William Shelukindo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
Abdallah S. Possi anakuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania – Umoja wa Mataifa Geneva Uswisi akichukua nafasi ya Balozi Maimuna Tarishi aliyemaliza Mkataba wake
Dkt. John S. Simbachawene anakuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uganda akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Aziz P. Mlima aliyestaafu.