The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aongeza Kiwango cha Mkopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu – (Video+Picha)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na ZAHLIFE kutoka Zanzibar pamoja na Wale wanaowakilisha Serikali za Wanafunzi kutoka Taasisi za Elimu ya Juu, Tanzania Bara na Zanzibar kwenye Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 11 Februari, 2023.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuongeza kiwango cha mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu maarufu kama ‘boom’ hadi kufikia shilingi 10,000 kwa siku.

Rais Samia amesema hayo Februari 11, 2023 wakati akizungumza na Wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na Zanzibar (TAHLIFE), Ikulu Chamwino Dodoma.

Awali, wanafunzi wa vyuo vikuu waliopata mikopo, walikuwa wakipewa shilingi 8,500 kwa siku.

Rais Samia amewataka Watanzania hususan vijana, kutokubali kulazimishwa mambo ambayo ni kinyume na mila na tamaduni za Kitanzania.

Rais Samia akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Adolph Mkenda wakati akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na ZAHLIFE kutoka Zanzibar mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 11 Februari, 2023.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wale wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), ZAHLIFE wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 11 Februari, 2023.

 

Leave A Reply