The House of Social Media
gunners X

Rais Samia Ashiriki Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala pamoja na Watumishi wa Serikali mara baada ya kuweka saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mtumba Mkoani Dodoma tarehe 30 Septemba, 2022.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki hafla utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo tarehe 30 Septemba, katika Jengo la Kitega Uchumi jijini Dodoma

Rais Samia akiweka saini moja ya mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe.
Rais Samia akionesha moja ya mikataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe mara baada ya kuusaini katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma tarehe 30 Septemba, 2022.
Wakuu wa Mikoa wakiweka saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe.
Wakuu wa Mikoa wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa saini mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 30 Septemba, 2022.


Leave A Reply