Rais Samia Atembelea Kwenye Kaburi la Rais wa Kwanza wa Malawi – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake huko nchini Malawi ambapo hii leo ametembelea na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Malawi na Baba wa Taifa hilo Hayati Dkt. Kamuzu Banda lililopo katika Makumbusho ya Kamuzu, Lilongwe nchini humo ambapo wakati akitoka kwenye makumbusho hayo alikutana na kusalimiana na Mama Cecilia Kadzamira ambaye alifanya kazi kwa karibu na Rais wa Kwanza wa Malawi na Baba wa Taifa hilo Hayati Dkt. Kamuzu Banda.

Pia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepanda mti nje ya Ofisi za Bunge la Malawi kama kumbukumbu wakati alipofanya ziara Ofisini hapo Jijini ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake iliyoanza hapo jana nchini Malawi.
Aidha, Rais Samia Suluhu bado yupo nchini Malawi akiendelea na ziara yake hiyo kufuatia mwaliko kutoka kwa mwenyeji wake, Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera kuhudhuria maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wan chi hiyo ya Malawi.


PICHA NA IKULU