The House of Social Media
gunners X

Rais Samia Atoa Heshima Za Mwisho Msiba Wa Marehemu Zelothe Stephen – Picha

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Zelothe Stephen Zelothe Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Oktoba 28, 2023 alifika kutoa heshima za mwisho nyumbani kwa aliyekuwa Kamishna Msaidizi mwandamizi (mstaafu) wa Jeshi la polisi nchni, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Marehemu Zelothe Stephen Zelothe Seaview-Upanga jijini Dar es Salaam.

Rais Samia akizungumza na Bi. Flora Zelothe Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Marehemu Zelothe Stephen Zelothe wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwake.
Rais Samia akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza la Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Marehemu Zelothe Stephen Zelothe.
Rais Samia  akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza la Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Marehemu Zelothe Stephen Zelothe wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023

NDEGE ILIYOBEBA MWILI wa MAREHEMU ZELOTHE ILIVYOTUA ARUSHA MBUNGE GAMBO NA RC MONGELA WAONGOZA

Leave A Reply