Rais Samia Awatakia Wakristo Kheri katika kipindi hiki cha Kwaresima

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatakia wakristo nchini kheri katika kipindi hiki cha kwaresima na kuwahimiza kutumia kipindi hiki kumuomba, Mwenyezimungu kutuoongoza katika kuishi kwenye ukweli na uadilifu.
“Nawatakia ndugu zetu Wakristo kheri katika Kipindi cha Kwaresima. Katika kipindi hiki cha siku arobaini za ibada, kufunga na kufanya toba, tuendelee kuiombea nchi yetu amani, upendo, umoja, utulivu na yote yaliyo mema, huku tukiwakumbuka wenye uhitaji.” —ameandika Rais Samia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.
“Tutumie pia kipindi hiki kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kutuongoza katika kuuishi ukweli na uadilifu kwenye utekelezaji wa majukumu yetu kwa wenzetu, na kwa nchi yetu.”—ameandika Rais Samia



Comments are closed.