Rais Samia Azindua Majengo ya Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar (Picha +Video)

ZANZIBAR – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi majengo mapya ya Taasisi ya Sayansi za Bahari (UDSM – IMS) Zanzibar, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya wahadhiri, watafiti, sekta binafsi, taasisi za serikali na jamii kwa ujumla.
“Ninawahimiza wahadhiri na watafiti kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi, taasisi za serikali na jamii kwa ujumla ili tafiti hizi zinazofanyika hapa ziwe na matokeo ya moja kwa moja kwa maendeleo ya wananchi,” alisema Rais Samia katika hafla hiyo.
Taaissi hii, iliyoko chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ina lengo la kukuza utafiti wa kisayansi katika masuala ya bahari, ikiwemo uhifadhi wa rasilimali za baharini, uvuvi endelevu, na maendeleo ya jamii zinazotegemea bahari. Rais Samia alibainisha kuwa matokeo ya tafiti haya yanapaswa kuleta faida halisi kwa wananchi wa Zanzibar na taifa kwa ujumla.






