The House of Favourite Newspapers
gunners X

Rais Samia: JWTZ Jiepusheni na Mashinikizo ya Kisiasa, Bakini Jeshi la Wananchi – Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla ya kufungua mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga tarehe 15 Desemba 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujiepusha na mashinikizo ya kisiasa, akisisitiza kuwa pamoja na umuhimu wa mshikamano kati ya uongozi wa kisiasa na uongozi wa kijeshi, jeshi hilo linapaswa kubaki huru na siasa za vyama.

Rais Samia amesema kuwa JWTZ ni jeshi la wananchi wote wa Tanzania na linapaswa kutekeleza majukumu yake kwa misingi ya uzalendo, nidhamu na utii kwa Serikali halali iliyopo madarakani, bila kuingizwa kwenye misuguano au maslahi ya kisiasa ya vyama.

Ameyasema hayo tarehe 15 Desemba 2025 alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi pamoja na Makamanda wa JWTZ, kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda, uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA), mkoani Tanga.

Katika hotuba yake, Rais Samia alieleza kuwa mshikamano na heshima kati ya uongozi wa kisiasa na uongozi wa kijeshi ni nguzo muhimu ya kulinda amani, umoja na usalama wa Taifa, huku akiwahimiza viongozi wa JWTZ kuendelea kulinda misingi ya katiba, weledi na maadili ya jeshi.

Leave A Reply