The House of Favourite Newspapers

Rais Tshisekedi Awataka Waasi wa M23 Kujiondoa Mara Moja Mashariki mwa DRC

0
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix Tshisekedi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix Tshisekedi, ametoa wito kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuwaamuru waasi wa M23 kujiondoa mara moja katika maeneo ya mashariki mwa Congo.

Akizungumza katika Global Gateway Forum lililofanyika jijini Brussels, Rais Tshisekedi alisema kuwa amani ya kudumu katika eneo la Maziwa Makuu haiwezi kupatikana bila kusitishwa kwa uingiliaji wa mataifa ya kigeni na mashambulizi yanayovuka mipaka.

Wito huo umetolewa wakati uhusiano kati ya Kinshasa na Kigali ukiendelea kuzorota, huku kukiwa na ongezeko la mvutano na hofu ya kuzuka upya kwa mapigano makali katika eneo hilo.

“Amani ya kudumu katika Maziwa Makuu haiwezi kufikiwa ikiwa tutapuuza mashambulizi yanayovuka mipaka na ushawishi wa kigeni,” alisema Rais Tshisekedi, akiashiria changamoto zilizopo katika mashariki mwa DRC.

Eneo la mashariki mwa DRC limekuwa likikabiliwa na migogoro ya kikabila na kisiasa kwa miongo kadhaa, huku vikundi vya waasi vikiendelea kuathiri usalama wa raia na shughuli za kibiashara katika mipaka ya Rwanda na Uganda.

VIDEO: KICHEKO cha TUNDU LISSU AKIWA NDANI ya MAHAKAMA LEO TENA – ASKARI MAGEREZA WAKIMUANGALIA..

Leave A Reply