The House of Favourite Newspapers
gunners X

RC Chalamila Afunguka: Tanzania Tumejifunza Morocco Kabla ya AFCON 2027

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema ofisi yake imetuma kikosi kazi maalum nchini Morocco kwa lengo la kujifunza namna taifa hilo lilivyojipanga na kuandaa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza uzoefu na maarifa ya kitaalamu katika maandalizi ya AFCON 2027, mashindano ambayo Tanzania itakuwa miongoni mwa waandaaji wakuu.

Chalamila amebainisha kuwa Morocco imepiga hatua kubwa katika masuala ya miundombinu, usafiri, usalama na uratibu wa mashindano makubwa ya kimataifa, hivyo ni mfano mzuri wa kujifunza kabla ya Tanzania kuingia rasmi katika maandalizi ya mwisho ya AFCON 2027.

Amesisitiza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una jukumu kubwa katika mafanikio ya mashindano hayo, hasa katika nyanja za mapokezi ya wageni, huduma za kijamii, usalama na miundombinu, hivyo kujifunza kutoka kwa nchi iliyofanikiwa ni jambo la msingi.

Leave A Reply