RC Kunenge Aungana na Wahindi Kuadhimisha Mwaka Mpya

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo ameshiriki hafla ya Mwaka Mpya wa Kihindu ambapo ametoa wito kwa Wahindi na wananchi kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha RC Kunenge ametoa Rai kwa wananchi wa Mkoa huo kulipa Kodi ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma Bora kwa Wananchi.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inasimamia suala la Amani na Utulivu Jijini humo ili kila mmoja aweze kufanya Shughuli zake kwa usalama.

