Real Wagoma kumuuza Asensio

REAL Madrid imeweka ngumu kwa Tottenham Hotspur kuwa hawana mpango wa kumuuza Marco Asensio. Tottenham inasemekana ilifanya mawasiliano na Real Madrid kuhusu uwezekano wa kumpata Asensio.
Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino kwa muda mrefu amekuwa na nia ya kumsajili Asensio. Mkurugenzi Mtendaji wa Real Madrid, Jose Angel Sanchez amesisitiza kuwa klabu yao haina mpango wa kumuuza staa huyo.
Sanchez alichimba mkwara kuwa klabu yoyote inayotaka kumnunua staa hiyo basi iwe tayari kutoa kitita cha pauni milioni 600 (Sh. trilioni 1.7). Naye Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane hataki kumwachia Asensio akiamini atakuja kusaidia timu hiyo katika siku za usoni. Asensio alijiunga na Real Madrid mwaka 2016 ambapo alisajiliwa kutoka Espanyol


Comments are closed.