The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ridhiwani Kikwete Aitaka Sekretarieti Ya Ajira Kuharakisha Kuweka Wazi Mchakato Wa Ajira 12,000 Zilizotangazwa Na Rais Samia

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameitaka Menejimenti ya Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuharakisha na kuweka wazi mchakato wa ajira 12,000 zilizotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 14 Novemba, 2025 jijini Dodoma.

Kikwete ameyasema hayo leo tarehe 24.11.2025 ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika taasisi hiyo tangu alipoapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Novemba, 2025 kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Amesema moja ya ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Utumishi wa Umma unakuwa bora katika kutekeleza majukumu ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuongeza kuwa ili kuhakikisha hili linaanza kutekelezwa aliahidi kutoa vibali vya ajira 12,000 kwa Kada ya Elimu watumishi 7,000 na Kada ya Afya, watumishi 5,000.

“Kibali cha ajira kimeshatolewa, nawashukuru kwa kuanza kufanyia kazi, ni jambo zuri, ni mategemeo yangu kuwa majawabu ya maelekezo ya Mhe. Rais tutayaona hivi karibuni, hakikisheni mnasimamia kwa ukamilifu, mchakato wote wa ajira hizi uwekwe wazi ili kuondoa dhana potofu ya kuwa kuna upendeleo katika kutoa ajira.” Mhe. Kikwete amesisitiza.

Ameitaka Menejimenti hiyo kuongeza kasi ya kuratibu mchakato wa ajira “Tuangalie changamoto zinazokwamisha uharakishaji wa mchakato wa ajira ili tuweze kutatua na kuendelea na kukamilisha kwa wakati.” Ameongeza.
Pia, ameielekeza Menejimenti hiyo kuzingatia maadili katika kusimamia mchakato huo wa ajira ili kuhakikisha wanapatikana watumishi sahihi na wenye vigezo. kwa maendeleo ya taifa.

Aidha, ameisisitiza Menejimenti hiyo kutoonea watumishi walio chini yao bali wawaelekeze kwa upendo. “Tusimamie maadili katika utekelezaji wa majukumu yetu, tusionee watumishi walio chini

Leave A Reply