Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake yanaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali mwilini yanayoweza kuwa sehemu yenye maumivu au sehemu nyingine mbali na maumivu yalipo.
Kuna Visababishi vingi ambavyo vinaweza kuwa vya kuhitaji matibabu ya haraka au sababu za kawaida. Pia maumivu yanaweza kuwa ya kuja na kuondoka au kudumu kwa muda mrefu.
Siku zote unapopatwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu unapaswa kufuatilia kwa kumuona daktari ili kufahamu kisababishi na kupata matibabu sahihi baada ya kupata vipimo, tiba na ushauri.
Visababishi vya maumivu ya tumbo chini ya kitovu huwa pamoja na Maumivu ya via (hasa sehemu ya mwisho ya utumbo mpana, rektamu, vya ndai ya peritoniamu, vya mfumo wa mkojo).
Maumivu hayo pia yanaweza kutokea kwa kujikunga kwa utumbo eneo lenye mishipa ya damu au kuwa na ugonjwa wa michomo kinga kwenye matumbo.
Lakini pia mawe kwenye miishio ya njia ya mkojo au maambukizi kwenye kibofu (U.T.I) ni sababu nyingine ya kuwa na maumivu hayo.
Visababishi vya maumnivu ya tumbo yanayoweza kusababisha kifo au kupoteza maisha ya mtuni endapo mgonjwa asipopata matibabu ya haraka.
Mtu anaweza kufariki ikiwa ana Maumivu makali ya kuziba kwa matumbo au Kutoboka kwa via ndani ya tumbo au Kuchanika kwa bandama/ini au utumbo kutokana na ajali bila kupata tiba ya haraka.
Mtu anaweza kufariki ikiwa ana homa kali ya tezi kongosho au Kupasuka kwa kifuko cha aota au Kuchanika kwa ujauzito ulotungwa nje ya kizazi bila kupata matibabu ya haraka.
Hitimisho: Upatapo maumivu ya tumbo chini ya kitovu ni vema kuwahi hospitali ili daktari akupime na akiona moja ya sababu tulizoziainisha atakutibu haraka. Kumbuka kuchelewa kupata tiba mapema ni kukaribisha kifo.

