The House of Favourite Newspapers
gunners X

Semina Kubwa ya Ujasiriamali Yazinduliwa Buchosa – Video

0

Kampeni ya elimu kwa mjasiriamali Jimbo la Buchosa imezimduliwa rasmi leo Mei 10, 2021, katika Kata ya Nyehunge ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Eric Shigongo ambayo aliitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

Semina hiyo inayogharamiwa na Mbunge Shigongo na inatolewa bure kwa wananchi wote wa Jimbo la Buchosa ambapo inasimamiwa na muelimishaji mahiri kutoka kampuni ya mjasiriamali Kwanza Enterprises, Dkt. Didas Lunyungu.

Mwanabuchosa na maeneo jirani njoo ujifunze jinsi ya kutengeneza, sabuni za aina zote, batiki, vijora, mishumaa, mafuta ya kupaka, keki za harusi, ufugaji wa kuku wa kienyeji na kuku wa kisasa.

Vingine ni kutengeneza vyakula vya mifugo, makapeti, mapambo ya sherehe, utengenezaji wa wine, sambusa, burger, piza, kilimo cha matikiti maji, nyanya, passion na mboga mboga.

Aidha, semina hiyo itafanyika katika kata zote 21 za Jimbo la Buchosa ili kuwawezesha wananchi kuinuka kiuchumi na kibiashara katika Jimbo hilo.

Leave A Reply