The House of Favourite Newspapers
gunners X

Serikali Yaipongeza CRDB kwa Kuimarisha Huduma za Kibenki Kidijitali

SERIKALI imeipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa Kongamano la Elimu ya Huduma za Benki kwa Njia ya Mtandao (Internet Banking), huku ikisisitiza kwamba teknolojia ni chachu ya mapinduzi ya kiuchumi duniani na kuwa Uwekezaji Katika TEHAMA sio tena jambo la hiari, bali ni la lazima kwa taasisi zote, ikiwa zinahitaji kumihili ushindani.

Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dk. Charles Mwamaja, wakati wa Kongamano hilo, huku akibanisha kuwa kielelezo cha umuhimu wa teknolojia ni Serikali nyingi duniani kuwa mstari wa mbele katika kutunga sera zinazowezesha matumizi ya teknolojia kwenye sekta mbalimbali ikiwamo ya fedha ili kuharakisha maendeleo. Dk. Mwamaja alisema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan nayo imeweka kipaumbele katika maendeleo ya TEHAMA kupitia sera mbalimbali zikiwemo Sera ya Taifa ya TEHAMA na Mpango Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano, unaosisitiza matumizi ya teknolojia katika sekta zote za uchumi, lengo likiwa kuhakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na mapinduzi ya kidijitali.

“Moja ya sekta zilizonufaika zaidi na mapinduzi haya ya teknolojia ni Sekta ya Benki, kwani katika miongo mitatu iliyopita tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye sekta hiyo. Katika hili CRDB imekuwa benki kiongozi katika kuboresha mifumo ya utoaji huduma ili kutoa huduma zilizo salama, rahisi, na za haraka kwa wateja.

“Teknolojia imewezesha upatikanaji wa huduma za fedha kwa wananchi wengi hivyo kuchochea Huduma Jumuishi za Fedha, ambazo sasa hivi zinapatikana kwa urahisi iwe kutuma na kuhamisha fedha, kulipia ankara mbalimbali, kulipia bima, na teknolojia imeenda mbali zaidi sasa hivi wananchi wanaweza mpaka kujifungulia akaunti wenyewe. “Serikali nayo imenufaika na mageuzi haya, ambapo tumeweza kuunganisha mifumo yetu kama GEPG (Government Electronic Payment Gateway), MUSE (Unified Social Economic Model), na TAUSI (Tanzania Automated Information System) na mifumo mbalimbali ya malipo ya kibenki ikiwamo ya CRDB,” alisema Dk. Mwamaja.

Aliongeza ya kwamba uunganishwaji huo umesaidia kuimarisha ukusanyaji wa kodi, tozo, na mapato mengine ya umma, huku akiipongeza CRDB kwa juhudi za kuboresha mifumo yake ili kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia, huku akiitaja benki hiyo kama iliyoonesha utayari mkubwa katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora na salama. “Kwa kuhitimisha, nawapongeza tena Benki ya CRDB kwa kuandaa kongamano hili na Wizara ya Fedha, kama msimamizi wa Sekta ya Fedha nchini, inavutiwa sana na programu hizi za elimu kwa kuwa matumizi sahihi ya mifumo hii ndiyo msingi wa uchumi wa kidijitali.

“Niwahakikishie kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia huduma za fedha za kidijitali kwa manufaa binafsi na ya uchumi wa Taifa letu,” alisema Dk. Mwamaja huku akiwapongeza washiriki wa kongamano hilo na kuwataka kutumia vema elimu waliyopata ili kujharakisha ukuaji wao kiuchumi. Naye Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Laballa, moja ya vipaumbele vya benki yake ni kuendelea kuongoza soko la bidhaa katika Sekta ya Fedha, lengo likiwa ni kukidhi matarajio na mahitaji ya wateja wao, hivyo uhakikisha wanaboresha mifumo yao ya huduma kila wakati ili kuhakikisha huduma rahisi, salama na nafuu kwa wateja

Alibainisha ya kwamba madhumuni makubwa ya kongamano ili ni kutoa fursa kwa washiriki kuuliza maswali yanayohusiana na huduma za kibenki kwa njia ya mtandao, ili wakawe mabalozi wazuri wa taasisi yake kwa jamii na klwamba kusanyiko hilo limelenga kubainisha fursa ilizonazo katika ‘internet banking.’

“Licha ya mageuzi na maboresho mengi tuliyoyafanya katika kipindi cha miaka 30 ya benki yetu kutoa huduma, sasa dunia inaenda kuhamia kwenye ulimwengu wa kidigitali kwa kuruhusu miamala isiyokuwa ya pesa taslimu ‘cashless transactions’ na hapo ndipo ‘internet banking’ na nyinginezo zinapochukua nafasi. “CRDB tumefanya mapinduzi makubwa kwenye malipo hapa nchini kwa makampuni na watu binafsi, biashara, taasisi za malipo. Kunma faida nyingi sana kwa wateja wetu wa CRDB kutumia ‘internet banking’ kwenye ulimwengu huu wa kidijitali, unaoruhusu biashara kufanyika kwa msaa 24 na bidhaa kuhuzwa mahali popote duniani na muuzaji kupata taarifa zake kiganjani.

“Kupitia huduma zetu za ‘internet banking’, mteja anaweza kuona salio lililoko kwenye akaunti yake, kupata taarifa za akaunti yake ‘bank statements,’ kuhamisha fedha kutoka katika akaunti yake ya CRDB kwenda akaunti nyingine ya CRDB au benki nyingine ya ndani au nje ya Tanzania, kwenda kwenye namba za simu na waajiri kuwalipa wafanyakazi mishahara.

“Kwa kufanya hivyo pia, maana yajke malipo serikalini yanaweza kwenda kwenye mfumo wa GEPG, kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kununua ama kulipia ankara muhimu kama luku, ving’amuzi, kulipia tiketi za usafiri ikiwemo ndege na manunuzi mengine ya kimtandao,” alisema Laballa mbele ya Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa CRDB, Bonaventura Paul.

Comments are closed.