The House of Favourite Newspapers
gunners X

Serikali Yazalisha Ajira Zaidi ya 1,400 Nje ya Nchi kwa Vijana na Wanawake

0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu

Serikali imefanikiwa kuzalisha ajira zaidi ya 1,400 za vijana na wanawake kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika kipindi cha mwezi Novemba 2025 hadi sasa ikiwa ni matokeo ya mahusiano mazuri yalipo kati ya Tanzania na nchi za nje ili kusaidia kupunguza tatizo la ajira.

Akizungumza wenye hafla ya kuwaaga vijana 109 waliopata fursa ya kazi katika nchi za ughaubini leo (08 Januari 2026) jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu alisema mafanikio hayo ni utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza ajira.

Tangu Novemba mwaka 2025 hadi Januari mwaka huu Serikali imefanikisha vijana 1,432 kwenda kufanya kazi nje ya nchi ikiwa ni matokeo ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kukuza mahusiano ya kidiplomasia na mataifa ya nje alisema Waziri Sangu.

Sangu alitaja mafanikio mengine ya Serikali kuwa ni pamoja na upatikanaji wa fursa za ajira 8,000 nje ya nchi ifikapo mwisho wa mwaka huu ambapo tayari nafasi za ajira 500 za madereva pikipiki zimetangazwa kwa nchi ya Falme za Kiarabu (UAE) na mchakato wa usaili utakamilika mwezi Februari mwaka huu.

Alitaja fursa nyingine ya ajira 50,000 nchini Japan za kukuza ujuzi kwa vijana kwenye kwenye sekta ya ujenzi ambapo majadiliano yanaendelea na yatakapokamilika vijana kote nchini watangaziwa kuomba.

Waziri Sangu aliwahakikishaia vijana hao 109 walioagwa leo kuwa Serikali imeratibu sula la mikataba yao, usalama wao na mazingira ya kazi wanapokwenda kupitia Mabalozi wanaowakilisha nchi hivyo amewataka waende wakafanye kazi kwa weledi, nidhamu na kudumisha mila za Kitanzania.

Akizungumza awali Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Zuhura Yunus alisema kwenda kufanya kazi nje ya nchi ni fursa nzuri ya ambapo tukio la leo kuwaaga vijana 109 ni uthibtisho wa lengo la Serikali kuzalisha ajira kwa makundi ya vijana na wanawake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala wa Ajira Tanzania Bara (TRAA) Abdallah Khalid Mohamed amesema ushirikiano kati yao na Serikali umefanikisha kupatika kwa fursa za ajira nje ya nchi na ndani kwa watanzania wengi.

Leave A Reply