The House of Favourite Newspapers
gunners X

Shilole Amlilia Rais Samia Ataka Sheria Mpya Mauaji ya Wanawake

0
Shilole mbali na Muziki lakini pia ni Mjasiriamali

SHILOLE au Shishi Baby; ni mwanamama anayefanya Bongo Fleva na mjasiriamali ambaye kuhusu kukithiri kwa mauaji ya wapenzi hasa wanawake, anamuomba Rais Samia kusaidia itungwe sheria mpya.

 

Shilole ambaye kipindi kile alieleza jinsi alivyokuwa akipokea kipigo kwa aliyekuwa mumewe, Uchebe amesema;

 

“Tunamuomba Rais atusaidie kutunga sheria mpya kwa ajili ya kumlinda mtoto wa kike kwenye ndoa na maisha ya kawaida ili tuondoe huu ukakasi.

 

Kwenye ndoa kuna matukio mengi makubwa yanatokea na watu hawasemi chochote mwisho wa siku anayeathirika ni mama.

Shilole anamuomba Rais Samia kufanya jambo kuwasaidia wanawake wanaonyanyasika katika ndoa zao

“Nipo kama mwanamke mtetezi wa wanawake wenzangu, nilikuwa namuomba Mhe Rais Samia Suluhu Hassan atusaidie kuunda sheria mpya inayomtetea mwanamke.”

 

Kumekuwa na matukio mengi yanayosababishwa na migogoro ya ndoa ikiwemo mauaji kutokana na kile kinachotafsiriwa kama wivu wa mapenzi hali inayotishia jamii na kuona haja ya kuwepo sheria rasmi ya kuratibu mahusiano ndani ya ndoa.

Leave A Reply