The House of Favourite Newspapers
gunners X

Shilole Apata Ajali Njiani Akitoka Kigoma Kurudi Dodoma

0

Msanii wa Bongo Muvi na mjasiriamali anayemiliki mgahawa maarufu wa Shishi Food, Zuwena Mohamed amepata ajali ya gari akiwa njiani kurudi Dodoma kutoka Kigoma, baada ya kushiriki shughuli ya kijamii ya Pilau Day iliyoratibiwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Babalevo.

Mbunge Babalevo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii amethibitisha tukio hilo.

“Jana usiku dada yangu Shilole alipokuwa anatoka Kigoma kurudi Dodoma alipata ajali ya gari aina ya Alphard baada ya kugonga ng’ombe maeneo ya Maragalasi. Tunafuatilia afya yake kwa ukaribu, kwa sasa anaendelea kupata matibabu Tabora,” alisema Mbunge.

RAIS SAMIA AGUSWA na VIFO 10 – MAJERUHI 23 wa AJALI ya GARI MOROGORO – ATUMA SALAMU za RAMBIRAMBI..

Leave A Reply