Simba vs Yanga Nusu Fainali FA – Video
SASA ni rasmi Simba na Yanga zitapambana kwa mara ya tatu msimu huu baada ya jana Simba kuifunga Azam FC na kutinga nusu fainali ya Kombe la FA.Awali Yanga na Simba zimepambana katika Ligi Kuu Bara mara mbili. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa sare ya 2-2, mechi ya pili Yanga ikashinda 1-0.
Sasa timu hizo zinakutana kwenye FA mchezo ambao utapigwa baadaye mwezi huu Uwanja wa Taifa.Simba katika mchezo wa jana uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar, mabao yao yalifungwa na John Bocco dakika ya 40 na Clatous Chama dakika ya 56.Mchezo wa jana ulikuwa na matukio mengi ndani ya uwanja ambapo mara kadhaa wachezaji walifanyiana ubabe.
Wakati mwamuzi akimaliza mchezo, kiungo wa Azam, Frank Domayo alionekana kumkanyaga beki wa Simba, Shomary Kapombe ambaye alianguka chini na kuondolewa na machela.
Kabla ya Simba jana haijapata ushindi huo, juzi Yanga iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Katika mchezo wa mapema wa hatua hiyo uliochezwa jana Jumatano kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wenyeji Sahare All Stars walitinga nusu fainali kwa kuichapa Ndanda penalti 4-3.
Mchezo huo ulimalizika dakika tisini kwa sare ya bao 1-1.Baada ya kutinga nusu fainali, Sahare itapambana na Namungo ambayo juzi Jumanne ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, iliifunga Alliance mabao 2-0.Wakati huohuo, kiungo wa Simba, Sharaf Eldin Shiboub ambaye alikwama kwao Sudan kipindi hiki cha corona, jana alirejea hapa nchini na moja kwa moja kwenda Uwanja wa Taifa kuwashuhudia wenzake wakiichakaza Azam FC.
Shiboub ambaye aliondoka tangu Machi, Morrison akisaini kitabu cha wageni….akiingia kwenye gari tayari kuondoka…akiwa na rafiki yake wakitoka ndani….akitoka kuhojiwa.mwaka huu baada ya ligi kusimama, amekuwa mchezaji wa mwisho wa Simba kuungana na wenzake kutokana na nchini kwao kufunga mipaka kwa muda mrefu ikiwa ni sehemu ya kujikinga na corona.
SHEREHE ZA UBINGWA SIMBA ZAANIKWA
Wakati Simba wakikata tiketi ya kufuzu nusu fainali ya Kombe la FA, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imetangaza kuwa, itaikabidhi Simba kombe lake la Ligi Kuu Bara msimu huu katika Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi watakapocheza dhidi ya Namungo, Julai 8, mwaka huu.