The House of Favourite Newspapers

Simba Wampa Masharti Mawili Morrison

0

UONGOZI wa Simba licha ya kumsamehe winga wao, Bernard Morrison, lakini wamepatia masharti ambayo anatakiwa kuyafuata baada ya kupewa msamaha huo ndani ya kikosi chao.


Morrison alisimamishwa ndani ya timu hiyo
kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu alivyoonyesha huku uongozi wa Simba ukimtaka mchezaji huyo kuandika barua ya maelezo kwenda kwa CEO wa timu hiyo, Barbara Gonzalez jambo ambalo Morrison alilitekeleza


Akizungumza na Championi Jumatano,
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally alisema kuwa
tayari uongozi wa
timu hiyo umepokea barua ya maelezo ambapo mchezaji huyo aliomba msamaha kwa maandishi na maneno baada ya kukutana na uongozi wa Simba ambao baada ya kumsamehe umempa masharti ya kuwa mfano mzuri wa kuigwa ndani ya timu hiyo na kutorudia vitendo vya utovu wa nidhamu.


“Jumatatu mchana Bernard Morrison
aliwasilisha barua ya msamaha kwa uongozi wa Simba ambapo alikutana na uongozi wa timu wakazungumza na Morrison alipatiwa msamaha na siku hiyohiyo alijiunga na wenzake na kuanza rasmi mazoezi.


“Katika msamaha ambao amepewa winga
huyo anatakiwa kuacha kufanya tena vitendo vya utovu wa nidhamu na kuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji wengine ambapo mwenyewe amekiri kuwa atafanya hivyo na kuwa mfano bora wa kuigwa na kucheza kwa kujituma ndani ya timu hiyo,” alisema kiongozi huyo.

STORI: MARCO MZUMBE NA LEEN ESSAU

Leave A Reply