The House of Favourite Newspapers
gunners X

Simba Yapunguza Bei ya Jezi Zote Msimu Huu wa Sikukuu!

0
Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally

Klabu ya Simba Sc kwa kushirikiana na JayRutty wametoa ofa ya punguzo la bei ya jezi zake katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya ambapo jezi zote za klabu hiyo sasa zitauzwa kwa Tsh 12000 tofauti na Tsh Tsh. 45,000 ilivyokuwa inafahamika.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Desemba 16, 2025 na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema bei hiyo ya punguzo ni kwa siku 45 kuanzia leo Desemba 16, 2025 hadi Januari 30, 2026 na kubainisha kwamba klabu hiyo inalenga kwenda na kasi ya dunia huku akiongeza kuwa inaendelea kupambana na jezi feki.

“Tuko hapa kuwatangazia Wanasimba wote Tanzania na duniani kwamba tumetoa punguzo la bei ya jezi kutoka Tsh. 45,000 hadi Tsh. 12,000. Ofa hii ya sikukuu ni kwa jezi zote, za ligi, za kimataifa na za watoto. Jezi za watoto zimetoka na sasa zinapatikana madukani.”- Ahmed Ally.

“Pamoja na kwamba tunatoa punguzo la msimu wa sikukuu lakini pia tunapambana na jezi fake. Kama Mwanasimba alikuwa ananunua jezi fake Tsh. 15,000 sasa jezi original ataipata kwa Tsh. 12,000. Uamuzi ni kwako Mwanasimba.”- Ahmed Ally

“Bei hii ya punguzo inaanza leo Desemba 16, 2025 na itakwenda hadi Januari 30, 2026 hivyo tuna siku 45 za ofa hii. Na kuna watu wanakwenda nyumbani sikukuu, usikubali kwenda mikono mitupu, nunua jezi za Simba uende na zawadi.”- Ahmed Ally.

UPEPO MKALI WAANGUSHA SANAMU MAARUFU ya STATUE of LIBERTY NCHINI BRAZIL…

Leave A Reply