The House of Favourite Newspapers
gunners X

Simba Yatambulisha Jembe Jipya Kutoka Nchini Ghana, Takwimu Zake Zinatisha

0
Augustine Okrah mchezaji mpya aliyesajiliwa na Simba kutokea klabu ya Bechem ya nchini Ghana

KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo mshambuliaji raia wa Ghana Augustine Okrah akitokea Bechem United.

 

Okrah amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wekundu wa msimbazi Simba.

 

Msimu uliopita akiwa na timu ya Bechem amecheza mechi 31 akifanikiwa kufunga magoli 14 na kutoa Assist 8.

 

Licha ya kucheza kama kiungo mshambuliaji, Okrah ana uwezo mkubwa wakutikisa nyavu.

Okrah anakuwa mchezaji wa pili wa kimataifa kujiunga na Simba SC msimu huu

Huyu anakuwa ni mchezaji wa pili wa kimataifa kutambulishwa na wekundu hao wa msimbazi akiungana na mshambuliaji mwingine kutoka nchini Zambia Moses Phiri.

 

Vilabu mbalimbali vimeendelea na harakati za kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu mpya wa 2022/2023.

 

Aidha klabu ya Simba inatarajiwa kuanza safari kesho ya kuelekea nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ambapo timu hiyo inatarajiwa kuweka kambi ya wiki nne kabla ya kurejea nchini Agosti 5, 2022.

Leave A Reply