Simba Yatangaza Kuachana Rasmi na Kocha Zoran Maki Pamoja na Wasaidizi Wake
KLABU ya soka ya Simba imetangaza rasmi kuachana na Kocha wake Mkuu Zoran Maki pamoja na wasaidizi wake katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram wa Klabu hiyo.
Akiwa na Simba Zoran ameiongoza kucheza katika michezo mitatu ya kimashindano ikiwemo mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wa jadi Yanga ambapo alipoteza kwa kufungwa bao 2-1 lakini pia michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC ambayo amefanikiwa kushinda yote


