The House of Favourite Newspapers

SIMULIZI YA KUSISIMUA: THE DARKEST HOURS(SAA ZA GIZA TOTORO)-28

0

MTUNZI: Hashim Aziz (Hashpower)

0719401968

ILIPOISHIA:

“Nataka unitoe upweke ndani ya moyo wangu,” alisema huku akijitoa kwenye mikono yangu, nikamshuhudia akilitoa lile gauni jepesi alilokuwa amevaa, cha kushangaza ni kwamba ndani hakuwa na kitu kingine chochote, kwa hiyo ni kama alijiandaa kuja kunijaribu, wakati msimamo wangu siku zote ni kwamba huwa sijaribiwi.

SASA ENDELEA…

Macho yangu yakatua kwenye kifua chake kilichojaa vizuri, nikalisogeza taulo langu, sasa tukawa saresare maua, macho yake yakatua kwa ‘kiranja mkuu’, akatabasamu na kunitazama.

“Kumbe wewe siyo mdogo kama nilivyodhani mwanzo,” alisema huku akimpapasa kiranja taratibu, jambo lililomkurupusha shetani wangu alikokuwa amejificha, kiranja mkuu akasimama wima kama mwanajeshi anayejiandaa kupiga saluti, nikaipitisha mikono yangu kwenye kiuno chake, akashtuka kidogo na kuanza kujinyonganyonga.

Haukupita muda, nikawa nimeshamuweka vizuri, naye akatii bila shuruti, kipyenga kikapulizwa kuashiria kuanza kwa mpambano usio na jezi wala refa.

Kweli ilionesha alikuwa na upweke wa hali ya juu ndani ya moyo wake, kwani alinipokea kwa bashasha za hali ya juu, nikaanza kufumua mashuti ya nguvu na kusababisha awe analalama kama mtu anayeonewa lakini wakati huohuo akinihimiza kuongeza kasi ya mchezo.

Basi tulikukuruka pale kisawasawa, japokuwa nilikuwa mgeni katika dimba hilo la kikubwa, mazoezi makali ya viungo niliyokuwa nafanya, ukichanganya na zile bia nilizokunywa, kiwango changu kilikuwa kikubwa kwelikweli mpaka Kezia mwenyewe akasalimu amri.

Ngwe ya kwanza ilipoisha, kila mmoja alikuwa hoi, Kezia akageukia upande wa pili akiwa hajiwezi kwa uchovu, na mimi nikageukia upande wa pili.

“Samahani kama uliona nimekudharau muda ule wakati mnafika, kweli wewe ni kidume cha shoka,” alisema Kezia kichovu huku akinigeukia na kunibusu, nikaachia tabasamu pana na kumbusu kwenye paji lake la uso.

“Nataka uwe mume wangu, kuanzia leo utakuwa mume wangu, sawa? Ukizingua nakutwanga risasi,” alisema kimasihara, tukacheka na kukumbatiana.

“Ahsante sana Snox, nakupenda mwenzio,” aliniambia kwa sauti ya kunong’ona. Sikumjibu kitu zaidi ya kuguna tu kwa sababu kiukweli sikuwa najua kama nampenda au la, kimsingi nilichukulia uhusiano wetu kama mapenzi ya kawaida tu.

Basi michezo ya hapa na pale iliendelea, Kezia akionesha kuchanganyikiwa kabisa na mimi, wakati tukijiandaa kwa ngwe ya pili, mlango wangu uligongwa kwa nguvu. Yaani huyo aliyegonga ungeweza kudhani tuna ugomvi naye kwa sababu akigonga kwa nguvu na kuutingisha mlango kwa nguvu.

Tukakurupuka pale kitandani na Kezia akaokota gauni lake na kukimbilia maliwatoni. Nikaenda kufungua.

“Hujasikia kengele?” mwanaume mwenye mwili mkubwa, aliyekuwa amevaa koti refu, alisema kibabe huku mkononi akiwa ameshika ile mikanda inayovaliwa na wanajeshi viunoni. Nikawa najiumauma kwa sababu ni kweli nilisikia kengele ikigongwa mara moja tu lakini hata sikuwa najua maana yake ni nini.

“Wewe ni mgeni?”

“Ndiyo!”

“Bahati yako, vaa nguo zako haraka elekea Goligotha,” alisema kibabe kisha akatazama saa yake huku akitingishatingisha ule mkanda wake.

“Nakupa dakika mbili uwe umeshafika.”

“Goligotha ndiyo wapi?”

“Mwenyeji wako ni nani hapa?”

“Bonta.”

“Hakukupa maelekezo?” alihoji mwanaume huyo na kabla sijamjibu chochote, kwa bahati nzuri Bonta naye alitokeza akiwa na wenzake, wote wakiwa wamevaa makoti marefu meusi.

“Gamutu, huyo ni mgeni niachie mimi ntamuelekeza,” alisema Bonta, naye kwa sauti ya kibabe ambayo sijawahi kumsikia akiitoa, Suma akageuka na kumtazama Bonta, wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha mwanaume huyo akanigeukia na kushusha pumzi ndefu, akaelekea kwenye mlango uliokuwa unafuatia.

“Mdogo wangu, jiandae tunaenda mazoezini,” alisema huku akinirushia mfuko wa plastiki, nikaudaka na kumtazama Bonta.

“Badilika fastafasta nakusubiri hapa nje,” alisema, nikawa bado sijaelewa. Sikuona sababu ya yule jamaa mwenye mwili mkubwa kuwa mkali kwangu kiasi kile wakati sikuwa najua chochote. Niliingia ndani na kuufungua ule mfuko, ulikuwa na koti refu jeusi na mabuti kama yale wanayovaa wanajeshi.

“Kezia alikuwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia maliwatoni, akionesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.

“Muda wa kazi umefika! Sijui akifika chumbani kwangu na kunikosa atanifanya nini.”

“Nani?”

“Si huyo Gamutu! Jamaa nuksi huyo, angeweza kukutandika na mkanda wa jeshi mpaka ukome,” aliniambia Kezia, sikumjali sana, nikabadilisha nguo harakaharaka na kuvaa suruari yangu na fulana, juu nikavaa lile koti na kumalizia na mabuti.

“Wakikuuliza chochote kuhusu mimi waambie hujaniona, ukitoka usifunge mlango tutakutana hukohuko,” alisema, nikamsogelea na kumbusu kwenye paji la uso, akatabasamu. Nikatoka nje ambako Bonta alikuwa akinisubiri na wale wenzake, tukaanza kuelekea upande wa pili ambako wala sikuwa nakujua.

Tulikatiza kwenye kama shamba fulani hivi la miti, tukatokezea upande wa pili, nikashtuka kutokana na nilichokiona.

Watu wengi walikuwa wamesimama kwa kujipanga mstari, wote wakiwa wamevalia makoti meusi na wakiwa wamesimama kikakamavu, kwa harakaharaka idadi yao ilikuwa ni zaidi ya thelathini, wanaume wakiwa ndiyo wengi huku pia kukiwa na wanawake wachache.

Watu walizidi kuongezeka na hesabu za harakaharaka, mpaka Gamutu mwenyewe anafika, kulikuwa na watu kama hamsini hivi. Alipofika tu, nilimuona Kezia naye akiwasili kwa kujifichaficha, akajichanganya kama vile alikuwepo.

“Hii tabia ya kuwa tunafuatanafuatana vyumbani baada ya kengele leo ndiyo mwisho. Siku nyingine sitawafuata na mkanda, nitakuwa nakuja na bastola,” alisema kwa sauti iliyojaa vitisho. Basi kilichofuata baada ya hapo, alianza kutugawa kwa makundi, yakapatikana makundi matano.

Tukaanza mazoezi, yeye alikuwa amesimama mbele kwa hiyo akawa anatuelekeza kwa vitendo kisha tunaanza kufanya kama yeye alivyofanya huku akipita na kutukagua.

Nilishangaa kugundua kwamba hata akina Bonta nao walikuwa na mbabe wao maana pale yeye ndiyo alikuwa ‘top’, wengine wote wakawa wanafuata maelekezo yake, hakukuwa na Bonta wala Jombi, wote tulikuwa chini yake.

Tulianza kwa pushapu, yeye kazi yake ikawa ni kusema tu ‘chini, juu, chini…’ kisha anapita kukagua kama kuna aliyekuwa anafanya mzaha. Tofauti na kule Kazimzumbwi ambako wengi wetu tulikuwa tukibabaika, pale kila mtu alikuwa fiti, pushapu zilipigwa kwa muda wa kama saa nzima.

Ilifika mahali mimi mikono ikawa imekufa ganzi kabisa lakini nikawa najikaza. Baada ya hapo, tulianza zoezi la kurukaruka vichura, tukaruka kwa muda mrefu mpaka nikawa nahisi kama mwili wangu unapoteza ushirikiano.

Hakukuwa na mtu aliyekuwa ‘analialia’ kuchoka, akabadilisha zoezi na sasa tukawa tunafanya ‘squats’, kwa wale wanaofanya mazoezi mara kwa mara watakuwa wanalijua hili zoezi, unajishika mikono kichwani au kiunoni halafu unakuwa unashuka chini mpaka unachuchumaa kisha unasimama.

Tulifanya zoezi hili kwa muda mrefu mpaka uzalendo ukaanza kunishinda. Mara kwa mara Bonta alikuwa akinitazama kuhakikisha kama naenda sawa na wenzangu, akawa ananipa ishara za kunitia moyo ambazo kimsingi zilinisaidia sana.

Baada ya hapo, alituamrisha wote kuingia kwenye jengo kubwa kama bwalo hivi, mle ndani mlikuwa kama ‘gym’, kulikuwa na vyuma vingi vya kufanyia mazoezi na vifaa vingine vingi, tukanyanyua sana vyuma zamuzamu huku akipita kukagua kwa karibu kuona kama kila mtu anafanya kile alichoambiwa.

Zoezi la mwisho, lilikuwa ni la ‘ku-craw’, haya mazoezi huwa wanayafanya sana wanajeshi, mnalala chini na kuanza kujivuta kwa kutumia tumbo huku ukitumia viwiko vya mikono.

Je, nini kitafuatia? Usikose kesho hapahapa! Unaweza pia kusoma au kusikiliza hadithi nyingine kwa kuingia: www.simulizizamajonzi7113.blogspot.com ,  Facebook: Simulizi za Majonzi au Youtube: Hashpower Online. Usisahau kulike, share na ku-subscribe.

 

 

Leave A Reply